ELIMU YA JINSIA

Elimu ya jinsia ni mafunzo maalum ambayo yametolewa na wataalamu kutoka mradi wa Youth Challenge International unaofadhiliwa na nchi ya Canada ambao pia unajulikana kwa jina la (EQUIP HUB). Elimu hii ambayo imefanyika tarehe 14/02/2017 na tarehe 21/02/2017, imehusisha suala zima la kujenga uelewa kwa wafanyakazi wa Mamlaka ya Mafonzo Amali wakiwemo maafsa, wakuu wa vituo na wasaidizi juu ya suala zima la muamko pamoja usawa wa kijinsia katika kutekeleza kazi ili kuwepo na ufanisi mzuri wa kazi. Pia imesisitizwa kuwe na ushirikishwaji wa jinsia zote mbili katika masuala ya kujenga maamuzi na shughuli zote za kuleta maendeleo katika kazi. Hali hii itasababisha kutoa mashirikiano baina ya pande zote mbili (Wanawaka na Wanaume) na kuimarisha utendaji utendaji pamoja na kuleta ufanisi mzuri katika kazi.