The Revolutionary Government of Zanzibar
VOCATIONAL TRAINING AUTHORITY

Mkurugenzi Mtendaji Dkt. Bakari Ali Silima akitoa maelezo katika warsha ya kazi ya kufanya tathmini kwa mafundi wazoefu (RPL), warsha ambayo ilifanyika leo tarehe 19/01/2025 katika chuo cha Mafunzo ya Amali Vitongoji kwa iliowashirikisha walimu katika fani nane, fani ya Magari, Upishi, Uchoraji na mapambo, Uashi,Ushoni, Elektroniki, Welding na Umeme. ambapo pamoja na kuifungua warsha hio pia aliwanasihi walimu hao na kuwasisitiza suala zima la kufanya uadilifu katika kuwapima mafundi hao, sambamba na hilo aliwataka walimu hao kuzingatia uwezo husika wa fundi katika kufanya tathmini ili waweze kuwapima mafundi hao na kuwapatia cheti kitakachoendana na ujuzi walionao. Nao walimu hao walizipokea nasaha hizo na kuahidi kuzifanyia kazi.

Scroll to Top